MUHTASARI WA MRADI

Mwongo uliopita umeshuhudia ongezeko la umiliki wa mashamba kwa uzalishaji wa vyakula, uzalishaji mali na maendeleo katika viwango vya ulimwengu. Sheria ya kimataifa inatekeleza majukumu mengi, wakati mwingine majukumu haya yanakinzana. Kwa upande mmoja, sheria inasawiri shamba kama bidhaa muhimu kupitia kwa biashara na uwekezaji, na kwa upande mwingine inatambua umuhimu wa mustakabali wake kama msingi wa maisha ya watu, utamaduni wao, mazingira, na hali yao kimaisha. Ingawa kuna utambuzi wa haki ya umiliki wa mali kwa wanajamii asilia, kupata haki kwa wanajamii wanaokumbwa na matatizo ya uharibifu wa mazingira yao asilia ulimwenguni kote imekuwa ni changamoto kubwa katika dunia nzima.

HAKI YA MALI (PROPERTY[IN]JUSTICE) (2020-2025) ni mradi wa utafiti unaochunguza jukumu la sheria ya kimataifa katika kuhakikisha haki kupitia kwa utungaji wa sheria zinazolinda haki ya umiliki wa shamba. Zaidi ya kufanya uchanganuzi wa desturi za kiutamaduni na kuhusisha mitazamo ya taaluma na tamaduni zinazoingiliana, mradi huu unalenga kupanua ufahamu wa mawanda ya milki na kutetea ufahamu zaidi wa mashamba kwa msingi wa kimaeneo katika sheria ya kimataifa. radi huu unafadhiliwa na Halmashauri ya Utafiti Uropa (European Research Council), unaratibiwa na Amy Strecker, na kutekelezwa katika Kitivo cha Uanasheria cha Sutherland (Sutherland School of Law), Chuo Kikuu cha Dublin (University College Dublin).

Katika kuchunguza jinsi sheria ya kimataifa inavyotekeleza haki kimaeneo kupitia kwa uelewa wake wa haki ya mali, mradi huu una malengo matatu makuu:

  1. Kuchanganua uungwaji mkono na utesi uliopo baina ya nyanja mbalimbali za sheria ya kimataifa zinazoathiri njia ya kufikia kwa shamba na kutathmini athari ya maeneo haya katika desturi ya nchi.
  2. Kutathmini matumizi na ubadilishaji wa kaida za kimataifa miongoni mwa wanajamii ili kupata shamba, kudai shamba au kukataa maendeleo yanayoathiri shamba lao; na
  3. Kutumia mitazamo ya taaluma na tamaduni zinazoingiliana kutetea ufasiri wa pamoja unaostahiki kuhusu milki katika shamba.

Unafanya hivi kupitia kwa miradi midogomidogo minne inayohusiana:

  1. Uainishaji mali (Amanda Byer, Utafiti wa baada ya shahada ya Uzamifu)
  2. Utatanishaji mali (Sonya Cotton, Mtahiniwa katika shahada ya Uzamifu)
  3. Uhusishaji mali (Raphael Ng’etich, Mtahiniwa katika shahada ya Uzamifu)
  4. Upanuzi mali (Amy Strecker, Mkaguzi Mkuu)

Sinéad Mercier ni Mtafiti Msaidizi katika mradi huu, naye Deirdre Norris ni Msimamizi wa Mradi huu.